PAROKIA NA UONGOZI

Parokia ya Kung’ara kwa Yesu Kristo, Mbezi Mshikamano ilitangazwa kuwa Parokia kamili na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo tarehe 26.04.2016 na Misa ya kwanza 01.05.2016. Parokia inasimamiwa na Mapadre wa Shirika la Wamisionari wa Africa (M.Afr.), kati ya
Mashirika matatu ya kwanza kuinjilisha nchini Tanzania. Awali msimamizi wa Parokia alikuwa Mt. Yohane Paulo II mpaka siku ya Kutabaruku Kanisa la Parokia katika
sikukuu ya Kung’ara kwa Yesu Kristo, 06.08.2023 ambapo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la D’Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi alibadilisha msimamizi kuwa
Kung’ara kwa Yesu Kristo. Paroko wa kwanza alikuwa Pd. Bartholomew Mrosso M.Afr) (2016-2018), akifuatiwa na Pd. Francis Kangwa (M.Afr) kuanzia 20.06.2018
hadi 13.04.2022 alipofariki dunia (Bwana ampe pumziko la milele). Pd. Louis Ntamati (M.Afr.) (Kaimu) kuanzia 15.04.2022 - 05.02.2023 na Paroko, Pd. Gilbert Bujiriri
(M.Afr.) kuanzia 05.02.2023 - 25.06.2023. Paroko, Pd. Protogene Rugwizandekwe (M.Afr) kuanzia 25.06.2023 akisaidiwa na Pd. Francis Xavier Angkosaala (M.Afr) na Pd.
Venance Bharotota (M.Afr) mpaka Julai 2024. Pd. Gilbert Bujiriri kuanzia Julai 2024 akisaidiwa na Pd. Venance na baadaye Pd. Theodore Ouedraogo (14.11.2024) na Pd.
Jean Paul Basikaba Evi (Aprili 2025). Parokia ina familia 642, waamini wote 2,807.

 

HALMASHAURI YA WALEI (2023-2026)


Halmashauri ya Walei inaundwa na Jumuiya 39 zilizogawanywa katika Kanda 11.
Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei Parokia iliyochaguliwa 19.02.2023 ni:
Mwenyekiti: Adam Kamanda
Makamu M.kiti: Alfred Tarimo
Katibu: Silvani Mng’anya
Katibu Msaidizi: Vitalis Mruma
Katibu Msaidizi: Alphonsina Ndunguru
Mtunza hazina: Eva Mushi