SALA KATIKA JUMUIYA NA KANDA
Mikutano ya sala katika Jumuiya hufanyika kila Jumamosi saa 12:30 asubuhi na
mikutano ya sala katika Kanda kila Jumamosi ya tatu ya mwezi, na ikiwepo
sababu ya kubadilisha itatangazwa kwa wakati. Kila Jumuiya na Kanda
inahimizwa kuadhimisha Misa kwa heshima ya wasimamizi wao.


MISA PAROKIANI NA KUABUDU EKARISTI TAKATIFU
Siku za Dominika huadhimishwa Misa tatu, saa 12:30, saa 2:30 asubuhi na Misa
ya watoto saa 5:00 asubuhi. Siku za sherehe na sikukuu au matukio muhimu
utaratatibu utatangazwa. Siku za wiki Jumatatu hadi Ijumaa Misa Takatifu
huadhimishwa saa 12:30 asubuhi zikitanguliwa na masifu saa 12:00 asubuhi.
Siku za Alhamisi ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu saa 11:00 jioni na kipindi cha
Kwaresma siku za Ijumaa Njia ya Msalaba saa 10:30 jioni ikifuatiwa na Misa
Takatifu. Kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi inaadhimishwa Misa kwa heshima
ya Moyo Safi wa Bikira Maria, saa 3:00 asubuhi baada ya sala za Jumuiya.


SAKRAMENTI
Sakramenti ya ubatizo hutolewa kila D o m i n i k a ya mwisho wa mwezi
katika Misa ya pili. Sakramenti ya Kitubio hutolewa kila Alhamisi wakati wa
kuabudu na siku za wiki baada ya Misa za asubuhi na kila mwaamini anapohitaji
upatanisho anaweza kumuomba Padre. Wagonjwa wanahudumiwa Ekaristi
Takatifu siku za Alhamisi na Dominika au pale inapohitajika kupitia Mapadre au
Wahudumu wa Ekaristi Wasio wa Kawaida.

MAFUNDISHO
Ekaristi (Komunio ya Kwanza) na Kipaimara ni kila Jumamosi saa 3:00 - 5:00
asubuhi; Jumatatu na Jumatano saa 10:00 – 11:30 jioni.
Wakatekumeni: Kila Ijumaa saa 3:00 asub. – 6.00 mchana.
Semina za ndoa: Kutegemea mahitahi na upatikanaji wa wahusika.
Mafundisho ya Dini Baada ya Kipaimara (MADIBAKI) – Utaratibu na ratiba
kamili itatolewa.


SEMINA, MAFUNGO NA HIJA
Ili kuhuisha imani Parokia itaandaa Semina, Hija na mafungo kwa makundi,
mashirika na vyama vya kitume hasa kwa vipindi maalum vya Kanisa kama
Majilio, Kwaresma, Pasaka, na wakati ufaao. Pia semina za pamoja kwa waamini
wote zitaandaliwa na kufanyika katika Dominika moja hasa ya tatu ya mwezi.